Mnamo Novemba 17, 2021, Balozi wa Tanzania nchini Marekani (Mhe. Elsie S. Kanza) aliratibu mazungumzo ya awali kwa njia ya mtandao ambayo yalimhusisha Balozi mwenyewe (akiwa Marekani) Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la kilimo Bw. Timoth mmbaga (akiwa Tanzania) na Mwakilishi wa shirika la SCI la Marekani Bi Ronda Pierce (akiwa Marekani). Mazungumzo hayo yalilenga namna ya kutumia vizuri fursa za kibiashara zilizopo kati ya Tanzania na Marekani kupitia mpango wa AGO.
Bi. Ronda ambaye pia ni mwakilishi wa SCI hapa Tanzania, alieleza kuwa siku za karibuni alitembelea Tanzania na kuona kuwa kuna fursa nyingi za kibiashara kati ya Marekani na Tanzania na kuwa SCI wako tayari kuratibu mchakato wa kuwaunganisha wanunuzi na watoa huduma nyingine wa Marekani na wale wa Tanzania kupitia Baraza la Kilimo na Ubalozi wa Tanzania Marekani. Aidha Mhe Balozi alieleza kuwa kwa sasa kuna mchakato wa kuandaa Jukwaa la Kibiashara kati ya Marekani na Tanzania katika kusherehekea miakaa 60 ya Uhuru wa Tanganyika na pia miaka 60 ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili na alitaman kuona Baraza la kilimo Tanzania linakuwa mstari wa mbele katika uratibu wa shughuli hiyo. Mkutano wa jukwaa hilo (Tanzania – USA Agribusiness Forum) utakaofanyika 7/12/2021 kwa njia ya Mtandao amabapo utakutanisha wadau (wafanyabiashara) kutoka Tanzania na Marekani na kutakuwa na mjadala mahsusi kwa kila kundi la mnyororo wa thamani uliopendekezwa hapa chini.
Baada ya mazungumzo pande zote (SCI, ACT na Ubalozi) walikubaliana kuanza na bidhaa chache ambazo ni.
- Parachichi hasa Mafuta ya parachichi (Avocado oil),
- Asali (Natural Honey),
- iii. Ufuta hasa mafuta yake (Sesame oil),
- Samaki na bidhaa zake (Fish and Fish Products)
- Bidhaa zitokanazo na zao la zabibu (Wine)
Mkutano huo uliazimia kwamba, Baraza za Kilimo Tanzania liratibu zoezi la kuwafikia wadau ambao wanajishughulisha na mnyororo wa thamani wa mazao hayo; kwa lengo la kutambua uwezo wa uzalishaji, aina ya bidhaa n.k
Ufuatoa ni mchakato wa zoezi hili;
- Novemba 24, 2021; Kuwasilisha orodha ya makampuni/taasisi/wakulima ambao wako tayari kunufaika na fursa ya kibiashara baina ya Tanzania na Marekani
- Novemba 29-30, 2012; Mkutano wa maandalizi kwa njia ya mtandao kati ya wadau waliojitokeza na wandaaji (ACT, Ubalozi na SCI ya Marekani)
- iii. Desemba 7, 2021; Kufanyika kongamano kubwa litakalojumuisha wadau mbalimbali kwenye mnyororo wa thamani wa bidhaa tajwa. Makongamano haya, yatafanyika kwa njia ya mtandao
Kwa Tangazo hili, Wanachama na wadau wengine ambao wako tayari kutumia fursa hii, tunomba wawasiliane na ACT Sekretarieti haraka iwezekanavyo kwa Bw. Khalid Ngasa Simu (whatsap) +255 683 343 716 barua pepe kngassa@actanzania.or.tz na nakala kwa Mkurugenzi Mtendaji wa ACT barua pepe tmmbaga@gmail.com, whatsap +255 6769969. Taarifa zihusishe jina, simu (whatsap), barua pepe, bidhaa unayoweza kuuza na kiwango au uwezo wako wa kuzalisha au kuuza bidhaa hiyo.