Na Mwandishi wetu. Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa (Mb) anatarajiwa kufungua Kongamano la Kilimo biashara (Agribusiness Forum 2020) linalotarajiwa kufanyika Feb
27 na 28 Jijini Dar es Salaam.huku kauli mbiu ikiwa ni “Kuongeza Tija katika Kilimo na Mifugo kwa Maendeleo ya Viwanda.” Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Bi. Jacqueline Mkindi imesena pia kongamano hilo linatarajiwa kuwaleta pamoja Mawaziri watano (5) ambao Wizara zao ziko kwenye mnyororo mzima wa thamani katika Sekta ya Kilimo. Katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam amewataja Mawaziri hao wanaotarajiwa kuhudhuria kuwa ni pamoja na Mh.Japhet Hasunga - Waziri wa Kilimo, Mh. Luhaga Mpina -Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Angelah Kairuki - Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji pamoja na Mh. Innocent Bashungwa Waziri wa Viwanda na Biashara na Mh. Issac Kamwelwe Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi. Kongamano hili liko wazi kwa wadau wote walioko kwenye Sekta ya Kilimo wa ndani na nje ya Tanzania, naomba kutumia fursa hii kuwaomba kujitokeza kushiriki katika kongamano hili kwa kujisajili ili kuthibitisha ushiriki wao kwa kutembelea tovuti ya Baraza la Kilimo Tanzania (Agricultural council of Tanzania www.actanzania.or.tz) hapo wataona link na watatakiwa kujisajili ili kushiriki kongamano. Tunatarajia kuwa washiriki zaidi ya 400. Kongamano hilo ambalo litaambatana na Maonyesho linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa kimataifa JNICC Dar es Salaam. Wadau wote wa Sekta ya Kilimo watakaoshiriki Kongamano hilo ni LAZIMA wajiandikishe kwa kujaza fomu iliyoko katika website ya www.actanzania.or.tz