Mkutano wa wadau wa Ubia wa Kilimo Tanzania December 2020- Nashera hotel

Stakeholders and cooperation partners meeting to launch PFS program.

Wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo wa kiwa katika mkutano wa wadau wa ubia wa Kilimo Tanzania. Warsha hii ilifanyika tarehe 10 na 11 Decemba 2020.

Programu hii inafadhiriwa na Serikali ya Norway, inatekelezwa ndani ya muda wa miaka 3 kuanzia Oktoba 2020 hadi Septemba 2023. 

programu hii wilaya 33( Mikoa 16) ambazo ni Tanganyika, Mpimbwe, Sumbawanga, Kalamboinatekelezwa, Mbozi, Kyela, Mbarali, Wanging’ombe, Mufindi, Iringa, Songea, Namtumbo, Tunduru, Masasi, Nanyumbu, Lindi, Ruangwa, Malinyi, Ulanga, Kilombero, Morogoro Rural, Mvomero, Same, Moshi, Meru, Monduli, kiteto, Kongwa, Bariadi, Maswa, Kishapu, Karatu, Babati

Lengo la PFS ni: Kuboresha Chakula , Usalama wa Lishe  na Kupunguza Umaskini.

 Matokeo ya PFS ni: Kuongeza Tija kwa Wakulima Wadogo; Kuongezeka kwa Fursa za kibiashara zinazoweza Kuendeleza uchumi na ajira kwa Watendaji wa Sekta Binafsi; na mifumo ya matumizi ya Kaya Kilimo Imeboreshwa.

Mpango huu utachangia lengo hili kupitia kuongeza usambazaJi wa  teknolojia  za kilimo kama Kilimo shadidi (SRI) na kilimo hifadhi (CA) na ubunifu ambao sio tu kunaongeza uzalishaji wa wakulima lakini pia uendelevu na uthabiti wa hali ya hewa.

Mradi huu utafanya kazi katika minyororo wa thamani wa  mazao saba (7) yaliyochaguliwa   ni Mchele, Mahindi, kunde, Pamba, Mtama, Ufuta na Alizeti.

Chini ya Progamu hii wadau takribani ya 366,900 kutoka Wilaya 33 (mikoa 16) wanatarajiwa kunufaika.